Skiza
Welcome
Login / Register

Halotel,Sport Pesa kunogesha michezo

Thanks! Share it with your friends!

URL

You disliked this video. Thanks for the feedback!

Sorry, only registred users can create playlists.
URL


Added by Admin in Sports
38 Views

Description

Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Halotel, imeingia katika makubaliano rasmi na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa ili kuongeza msisimko na ushiriki kwa wadau wa michezo ya kubashiri nchini.
Ushirikiano huo utawawezesha wateja wanaotumia mtandao wa Halotel kupitia kupidia huduma ya kifedha ya HaloPesa watapata nafasi ya kucheza, na kubashiri michezo mbalimbali na SportPesa kama ilivyo kwa mitandao mingine ya simu.Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya Ofisi za Halotel, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Halotel, Mhina Semwenda alisema, “Ushirikiano huu baina ya kampuni yetu na SportPesa utawawezesha wateja wetu kuweza kufurahia kushiriki katika michezo mbalimbali ya tofauti na huduma za kifedha za kawaida, kupitia simu za mkononi tofauti na miamala ya kawaida”

“Hii ni hatua ya kwanza kwa kampuni ya mawasiliano ya Halotel Tanzania na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa Tanzania kuingia katika mkataba wa makubaliano na ushirikiano ambapo wateja wa Halotel nchi wataweza kushiriki katika michezo ya kubashiri na kuweza kunufaika na fursa mbalimbali za kuboresha maisha yao kupitia zawadi watakazopata kupitia michezo hiyo ya kubahatisha”.

“Mtandao wetu umeenea Zaidi katika maeneo ya vijijini, jambo ambalo sasa litatoa fursa mpya ya ushiriki katika michezo kwa wateja wetu, ambao kwa namna moja ama nyingine walikuwa hawapati fursa hii ya kushiriki tunaamini sasa vijiji zaidi ya 4000 vitaweza kushiriki katika michezo ya kubashiri kupitia Sports Pesa, Alisema Mkuu huyo wa Mawasiliano na kuongeza.
“hii ni fursa kwa wateja wetu wote wa Halotel mijini na vijijini kuweza kushiriki katika michezo ya kubashiri kama vile mpira wa miguu, mpira wa kikapu, Rugby, Cricket na Tennis ambapo hapo kabla hawakuweza kushiriki katika michezo hii kwa kupitia mtandao wa Halotel(HaloPesa) wenye mawakala zaidi ya elfu 50,000, Alihitimisha Semwenda.
Aidha kwa upande wake, Afisa Uhusiano wa kampuni ya SportPesa Sabrina Msuya alisema “Hii ni nafasi nzuri kwetu na kwa wateja wa Halotel kwani tulikuwa tunapokea maombi mengi juu ya uhitaji wao wa kushiriki kucheza na SportPesa kama ilivyo kwa mitandao mingine.“Wateja wa HALOTEL wanatakiwa kutuma neno GAME kwenda namba 15888 ili kujisajili, ili aweze kucheza na SportPesa anatakiwa kuanza kwa kuweka pesa kwenye akaunti yake ya SportPesa kwa kupiga namba *150*88#, kuchagua lipa bili na Halopesa, kisha chagua 4: Michezo ya kubahatisha ambapo namba moja ni Sportpesa (150888) kisha namba ya kumbukumbu ambayo ni 888, kisha ataweka kiasi pamoja na namba ya siri ili kumaliza kujisajili”.Ushirika na Halotel umekuja wakati muafaka ikiwa ni wiki tatu tu tangu kampuni hiyo ambayo ni wadhamini wa vilabu vya Simba, Yanga na Singida United kutambulisha promosheni yake mpya ijulikanayo kama SHINDA NA SPORTPESA ambapo wateja wa SportPesa wanapata nafasi ya kuingia kwenye droo ili kujishindia zawadi mbalimbali kama bajaji aina ya TVS KING DELUXE, Jezi orijino ya Uingerezapamoja na safari ya kwenda Uingereza kushuhudia moja kati ya timu inayodhaminiwa na kampuni ya SportPesa(Everton, Hull City, Southampton na Arsenal) na kutuma neno SHINDA kwenda 15888 mara baada ya kuweka ubashiri wako.

Post your comment

Comments

Be the first to comment
RSS